Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa katika
usafishaji wa mazingira katika hosteli za chuo hicho mapema hii leo
Wanafunzi
hao wametoa wito kwa jamii nzima kusafisha mazingira yanayowazunguka ili kuepukana
na magonjwa mbalimbali ya mlipuko na kuungana na kauli ya Raisi ya
usafishaji mazingira
Hata hivyo
wanafunzi hao wameuomba uongozi wa chuo kuwapatia vifaa vitakavyo wawezesha
kusafisha mazingira yanayowazunguka kwa wakati swala ambalo pia litasaidia
taaluma ya chuo hicho kuongezeka kiwango
Aidha
wananchi wanao zizunguka hosteli za chuo hicho wamewapongeza wanafunzi hao kwa
jitihada zao katika usafishaji wa mazingira ya eneo hilo
‘kwa kweli na wasifu
wanafunzi wa chuo hichi kwani wamekuwa mfano mzuri kwa jamii hususani kata hii
ya olasiti kwa jitihada za usafishaji na
utunzaji mzuri wa mazingira yao’ Alisema Bi Salma Rashidi ambaye ni mmoja kati ya
wakazi wa eneo hilo