Tuesday 3 January 2017

UVCCM Wilaya Ya Longido Washerehekea Sikukuu Ya Mwaka Mpya Kwa Kuwatembelea Watoto Yatima - Namanga.

Mjumbe  wa Baraza kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN  Kaseko akitambulisha vijana wenzake wa UVCCM Wilaya ya Longido aliofuatana nao baada ya kuwasili katika kituo cha Watoto Yatima Maasai Foundation walipokwenda kuwatembelea jana tar. 01/01/2016

 *******
Jana tarehe 01/01/2017  katika kusherehekea sikukuu ya Mwaka mpya,  UVCCM Wilaya ya Longido wametembelea watoto Yatima Wanaolelewa na kituo Cha Masai Foundation Kata ya Namanga wilayani humo.
Akiongea kwa niaba ya UVCCM, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN  Kaseko ambaye pia ameongoza vijana wenzake amesema; "Sisi kama UVCCM tunatambua Serikali yetu ina mambo mengi sana ya kufanya kwa ajili ya Watanzania hivyo wakati mwingine sisi wenye mapenzi mema na Nchi yetu ni vizuri kuisaidia Serikali ili kuipunguzia majukumu na kuipa nafasi ya kufanya mambo mengine. 

"Hatuwezi kuiachia serikali peke yake ili ifanye mambo haya, Vijana huliinua na Kulijenga Taifa  hivyo Vijana ni lazima kujitoa kwa hali na mali ili kulitumikia Taifa letu kila mmoja kwa nafasi yake. 

"UVCCM Wilaya ya Longido tunaunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani kiukweli Serikali ya JPM imejikita na imedhamiria kwa dhati kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.

Ndg. Kaseko amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto waishio katika mazingira magumu linalohusisha yatima,vibaka na watoto wa mitaani na zipo sababu kadha wa kadha zinazochangia tatizo hili kama vile kufululiza kwa Ugomvi kwa wanandoa katika familia hupelekea watoto kukimbia familia zao, Ugumu wa maisha husababisha baadhi ya wazazi kukimbia familia zao na kuacha watoto kutawanyika na kukimbilia mtaani, Vijana wadogo kujiingiza katika Mapenzi kabla ya wakati sahihi na mapenzi yakikolea husababisha Mimba zisizotarajiwa na kwa sababu hakuwa na maandalizi hupelekea tatizo hili n.k 

"Tunaiomba serikali  iendelee kuvisaidia vituo kwa kulea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kwani nao ni binadamu kama sisi na wanahitaji kupata haki zao za msingi kama kupewa elimu ( shule ), kuishi vizuri, kula vizuri n.k  na sisi vijana tunaahidi kushirikiana  barabara na serikali  katika kutatua changamoto za wananchi wake.
"Nawashukuru sana vijana  wenzangu wa CCM Wilaya ya Longido kwa kujitoa kwa hali na mali ili kufanikisha hili." Alihitimisha  Kaseko


Vijana wa UVCCM wilaya ya Longido wakiwa Katika picha ya pamoja wakati wakikabidhi vitu mbalimbali kama zawadi kwa Watoto Yatima wanaolelewa na Kituo cha Masaai Foundation Kilichopo Namanga Wilaya ya Longido.


Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Longido Ndg. Tunu Lemanga akiongea baada ya kukabidhi kiasi chaTsh. 100,000/= ikiwa ni kuanza kutimiza ahadi yake aliyoitoa jana ya kuwakatia Bima ya Afya Watoto hao kwa Muda wa Mwaka Mmoja.

Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Robert PJN Kaseko ( Mwenye tshirt ya Kijani ), na Vijana wengine wa UVCCM Wilaya ya Longido wakiwa katika Picha ya Pamoja na sehemu ya Watoto yatima Walipotembelea Kituo cha Maasai Foundation jana tar. 01/01/2017
Katibu Hamasa wa UVCCM Mkoa wa Arusha Neema Kiusa akiteta na Watoto Yatima wanaolelewa na Kituo hicho Maasai Foundation mara baada ya UVCCM Wilaya ya Longido kuwatembelea na kushiriki kusherehekea pamoja na watoto hao sikukuu ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2017.

No comments:

Post a Comment